Friday, 26 September 2014

CRISTIANO RONALDO KUIGHARIMU MANCHESTER UNITED PAUNI MILIONI

    Cristiano Ronaldo scored another hat-trick for Real Madrid this week to take his goal tally to 264
GHARAMA halisi ya kumrejesha Cristiano Ronaldo Premier League inatajwa kuwa ni zaidi ya pauni milioni 140 huku pia ikigundulika kuwa washauri wa nyota huyo wa zamani wa Manchester United mkali huyo alipwe mshahara wa pauni milioni 20 kwa mwaka.
Inaelezwa kuwa Ronaldo hana amani Real Madrid na angependa kusikiliza ofa za kuondoka Bernabeu huku kocha wa Manchester United Louis van Gaal naye akishindwa kukanusha nia yake ya kumtaka mchezaji huyo bora wa dunia.
Hata hivyo klabu yoyote itakayomtaka Ronaldo italazimika kutoa mkwanja wa nguvu baada ya kubainika kuwa wawakilishi wa mchezaji huyo walitaka mshahara wa pauni 385,000 kwa wiki wakati alipotingisha kibiriti miezi 18 iliyopita.
Katika kipindi hicho, United chini ya David Moyes ilitaka saini ya Ronaldo ambapo familia ya Glazer ilikuwa imedhamiria kumrejesha nyota huyo lakini dili likashindikana.
Ronaldo akazivutia timu kadhaa barani Ulaya kabla ya kuamua kusaini mkataba mpya wa miaka mitano Bernabeu.  

No comments:

Post a Comment