#Exclusive: Diamond Platnumz azungumza kwa mara ya kwanza mambo 6 kuhusu fujo zilizotokea Ujerumani
Kuanzia siku tatu zilizopita stori kubwa kwenye kiwanda cha burudani Tanzania imehusu fujo zilizotokea Ujerumani kwenye show aliyokwenda kufanya Diamond Platnumz huko Stuttgart.
Kilichotokea ni kwamba saa kumi alfajiri ndio promota alimpeleka Diamond kwenye ukumbi kunakofanyika show. Kwa nini ilitokea akamchelewesha? nini kilitokea baadae? hizi hapa chini ni kauli za Diamond mwenyewe kwenye exclusive na
1. ‘Mpaka sasa hivi nashindwa kuelewa tatizo lilikua nini, siamini kama tatizo lilikua ni hela, balance iliyokua imebaki ni balance ndogo kama EURO 3500 hivi ambazo ni zaidi ya milioni 7 za Tanzania, ninavyojua Mapromoter wengi wa nje wakifanya show huwa wanauza na vinywaji wenyewe na wanapata hela nyingi sana kwenye vinywaji kuliko hata viingilio so nahisi labda walivuta muda ili waendelee kuuza vinywaji zaidi’
2. ‘Walichelewa kunipeleka kwenye show, walinifata kwenye mida ya saa tisa usiku na wakawa hawana hela yangu iliyobaki, nikawaambia siendi kokote mpaka wamalize kunilipa, walikua na EURO 1500 wakati nilikua nawadai 3500 nikawaambia lazima wanipe hela yote, wakaifata ndio tukaenda kwenye show’
3. ‘Tukafika kwenye show saa10 kasoro, kweli hata ningekua mimi shabiki ningekasirika ningefanya vurugu, wengine walilipa zaidi ya laki moja na wametoka kwenye miji na nchi jirani, niliwaambia wanipeleke nikafanye show ndani ya ukumbi japo tulikuta watu wengi sana nje lakini Mapromota walikua waogawaoga kunipeleka ndani’
4. ‘Nikakuta watu wengi na vurugu nje, nikamwambia promota atupeleke ndani tungefika kwenye stage ingetulia baada ya sisi kuimba manake ni vitu tunakutana navyo kwenye muziki lakini promota walikua waogawaoga, askari wa Ujerumani karibu gari 7 wakaja pale lakini mtiti ukawa mkubwa’
5. ‘So dakika ya mwisho tukaona hapashukiki ndio wakaturudisha hotelini, kiukweli nimesikitishwa sana manake nilikua nimejipanga vizuri na ilikua ni mara yangu ya kwenda kuperform pale Stuttgart, imenisikitisha manake watu walikua kuniona alafu mwisho ikashindikana kuwafikishia walichokitarajia’
6. ‘Nafikiri October tutakua na show nyingine na itafanyika kulekule, nilikua nazungumza na uongozi wangu kwamba wanataka show nyingine na tayari wameshatuma hiyo hela ya show nyingine’
Unaweza kumsikiliza Diamond mwenyewe kwa kubonyeza play hapa chini.
No comments:
Post a Comment