Wednesday, 24 September 2014

UKATILI: AMUUA MKEWE KWA KUMCHINJA

Jeshi la Polisi mkoani Katavi linamtafuta mkazi mmoja wa kijiji cha Urwila wilaya ya mlele anayetuhumiwa kumuua mkewe kwa kumchinja
kamanda wa polisi mkoa wa katavi dhahir kidavashari

Jeshi hilo limemtaja mtuhumiwa kuwa ni Bw. Mohamed Katyukulu mwenye umri wa miaka 49
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi Bw. Dhahir Kadavashari amemtaja aliyeuawa kuwa ni Bi. Bernadeth Mtweweli mwenye umri wa miaka 38 ambaye mumewe alikuwa akimtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine. 

No comments:

Post a Comment