Shirika la afya duniani- WHO, limesema mlipuko wa ugonjwa wa ebola
nchini Nigeria na Senegal unaonekana kwisha ingawa idadi ya vifo katika
maeneo hayo kutokana na ugonjwa huo imefikia 2,800.
Ripoti kutoka ofisi ya WHO huko Afrika imesema hakuna kesi mpya za
ugonjwa wa ebola zilizoripotiwa kutoka Nigeria tangu Septemba nane na
hakuna hata moja nchini Senegal tangu kesi ya kwanza ya pekee katika
nchi iliporipotiwa Augusti 29.
Imesema milipuko katika nchi zote umedhibitiwa. Ripoti tofauti ya WHO
imesema nchi za Guinea , Liberia, na Sierra leone zinaendeelea kuripoti
kesi mpya za ugonjwa wa ebola.
Imesema idadi ya kesi huko afrika magharibi imeongezeka kufikia 5,864 na idadi ya vifo imeongezeka kufikia 2,811.
No comments:
Post a Comment