Wednesday, 17 September 2014

KIWANDA CHA KUYEYUSHA MADINI YA SHABA CHA TPM KUWANIA TUZO YA RAIS YA HUDUMA ZA JAMII NA UWEZESHAJI



Mkuu wa wilaya ya Mpanda, Paza Mwamlima akizungumza na timu ya majaji na sekretarieti iliyomtembelea ofisini kwake kabla ya kufanya ziara katika kiwanda cha kuyeyusha madini ya shaba cha TPM kilichopo katika wilaya ya Mpanda mkoani Katavi.
Mtaalamu katika kiwanda cha kuyeyusha madini ya shaba cha TPM Mhandisi Innocent Mushi (kulia) akielezea jinsi mashine ya kuponda mawe yenye dhahabu (pichani) inavyofanya kazi kwa majaji na sekretarieti iliyofanya ziara katika kiwanda hicho ili kufanya tathmini ya kiwanda hicho katika utekelezaji wa miradi ya jamii kwa kipindi cha mwaka 2013.
Mmoja wa wachimbaji wadogo, Abraham Meshack ( wa saba kutoka kulia) akielezea jopo la majaji na sekretarieti mchango wa kiwanda cha kuyeyusha madini ya shaba cha TPM katika uwezeshaji wa kikundi chao katika ununuzi wa mashine ndogo kwa ajili ya kusaga na kuchenjua mawe yenye dhahabu.

No comments:

Post a Comment