Wednesday, 24 September 2014

KUELEKEA SIKU YA WAZEE:WAZEE WAKATAVI WALALAMIKIA HUDUMA ZA AFYA

Baadhi ya wazee wilayani Mpanda Mkoani Katavi wameeleza kukumbwa na changamoto mbali mbali ikiwa ni pamoja na Huduma duni za afya,kutozwa fedha wakati wa matibabu na Ukosefu wa miradi ya maendeleo hali inayowakosesha fursa za kimaisha

Hayo yameelezwa na Katibu wa umoja wa wazee mkoani Katavi Marius Bagaya wakati akizungumza na Sauti ya Katavi Mjini Mpanda kuhusu maandalizi ya sikukuu ya wazee ambayo kitaifa itafanyika mkoani humo
 
Mzee Bagaya amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kufanyika Oktoba mosi mwaka huu,ambapo yatatnguliwa na Kongamano la wazee litakalowakutanisha zaidi ya wazee 400 kutoka nje ya mkoa wa Katavi.            

No comments:

Post a Comment