Diamond Platnumz amerejea tena kwenye msimu wa
pili wa kipindi cha Coke Studio Africa na awamu hii
atatangeneza pair na hitmaker wa Johny, Yemi
Alade kutoka nchini Nigeria.
Diamond na Yemi Alade
Diamond ni msanii wa nne mwaka huu kutoka
Tanzania aliyeshiriki kwenye kipindi hicho
kinachorekodiwa jijini Nairobi, Kenya. Wengine ni
Vanessa Mdee aliyerekodi na Burna Boy wa Nigeria,
Joh Makini aliyerekodi na Chidinma wa Nigeria na
Shaa aliyerekodi na Jacky Chandiru wa Uganda.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Yemi aliyekuja
nchini mwaka huu ameweka picha akiwa na
Diamond katika studio hizo na kuandika:
#wonderment! With the infamous ubertalented six-
abbs superstar Diamond….@diamondplatnumz
#iAmHumbled #thankYouCokeStudio, ForThe
Opportunity God bless AFrica.. #cokeastudioafrica
@cokestudioafrica @dresomes Nosa @chocolatecity
Diamond has been singing your song all morning
@audumaikori.
Naye Diamond katika picha akiwa na mrembo huyo
ameandika:
Na dem ake Johny @yemialade , ushaelewa nini
kinaendelea si eti????….. (jus me and Johny’s
Girlfriend…You allready know what it is ryt???… Cc
@yemialade
No comments:
Post a Comment