Monday 20 October 2014

JWTZ ITOE TAMKO JUU YA DIAMOND NA NEY WA MITEGO KUVAA SARE ZA JESHI NA KUKATA MAUNO

 
Kama wiki mbili zimepita toka jeshi letu pendwa litupige mkwara juu ya matumizi ya sare zake au zinazofanana na hizo kwa mtu ambae si askari.. Kwamba ukivaa tu basi umevunja sheria na inapaswa uadhibiwe mara moja, either mahakamani au 'wapigwe tu'.. Hilo linapewa nguvu na taarifa ya juzi kati jamaa kulazimishwa kuoga maji ya barabarani maeneo ya kariakoo baada ya mjeda mmoja kumnyaka na nguo zinazofanana na zao.. 

Sasa cha ajabu mbona juzi katika tamasha la Fiesta mwanamziki Diamond na timu yake pamoja na Ney anayewatega, wameonekana wazi wakiwa na sare hizo tena wamezivaa hovyo hovyo kata K wakinengua jukwaani.??? Au hiyo sheria inamgusa nani?

Huyu kijana akiwa na ufahamu kuwa television ya taifa inaonyesha hili tamasha lao kavaa SARE ZA JESHI tena full kuanzia viatu mpaka kofia.

Wasanii ni Mfano wa Kuiga, Sasa hawa wanafundisha nini watu wengine?

Hii ni Dharau

No comments:

Post a Comment