Monday 20 October 2014

Serena Aonyesha Hasira Dhidi Ya Raisi Wa Tennis



Bingwa wa michuano ya US Open mwaka 2014, Serena Jameka Williams ameonyesha kukasirishwa na kauli iliyotolewa na rais wa shirikisho la mchezo wa tenisi nchini Urusi Shamil Tarpischev dhidi yake na dada yake Venus Ebony Starr Williams.
Serena amesema kauli iliyotolewa na kiongozi huyo wa nchini urusi imedhihirisha ubaguzi pamoja na kutojali jinsia.
Tarpischev amenukuliwa na vyombo vya habari akisema wazi kwamba dada hao kutoka nchini Marekani ni “Akina Kaka Wawili” kwa lugha ya kigeni alitamka William’s Brothers.
Hata hivyo kufuatia kauli hiyo isiyo na mantiki iliyotoka kinywani mwa kiongozi huyo imemsababishia kutozwa faini pauni 15,500 na kufungiwa kwa muda wa mwaka mmoja kutojihusisha na mchezo wa tennis.
Kauli ya Tarpischev, pia imeshutumiwa na shirikisho la mchezo wa tenisi duniani WTA pamoja na shikisho la mchezo huo nchini Marekani USTA

No comments:

Post a Comment