Wednesday 8 October 2014

PIGO ARSENAL, OZIL NJE HADI 2015 BAADA YA KUUMIA GOTI


KLABU ya Arsenal imepata pigo baada ya kiungo wake, Mesut Ozil kuumia na anatakiwa nje kwa kipidi chote kilichobaki kumaliza mwaka 2014.
Kiungo huyo alikwenda kufanyiwa vipimo vya MRI katika goti lake na Chama cha Soka Ujerumani kimethibitisha atakuwa nje kwa miezi mitatu.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 hakufanya mazoezi na timu yake ya taifa ya Ujerumani mjini Frankfurt baada ya kuanza kulalamika juu ya hali yake.
Mesut Ozil atakuwa nje kwa kipindi chote kilichobaki mwaka 2014 baada ya Chama cha Soka Ujerumani kuthibitisha kuumia kwake goti

Ozil hajaonyesha dalili kubwa za maumivu katika miezi ya karibuni na amecheza mechi tisa msimu huu, akifunga bao moja.
Taarifa ya Arsenal imesema: "Ozil alilalamika kuwa na maumivu ya goti la kushoto baada ya mechi na klabu ikakishauri Chama cha Soka Ujerumani kumfanyia uchunguzi atakapojiunga na kikosi cha timu ya taifa.
"Klabu itamfanyia uchunguzi wa kina na ni mapema sana kusema Ozil atakuwa nje kwa muda mrefu kiasi gani".



">Ozil, aliyesajiliwa kwa Pauni Milioni 42.5 mwaka jana, amekuwa akikandiwa kwa kucheza chini ya kiwango akiwa na jezi ya Arsenal. 
Habari za kuumia kwake zinazokuja mwezi wa pili ndani ya msimu mpya, ni pigo kwa kochaa Arsene Wenger ambaye sasa idadi ya majeruhi inaongezeka katika timu yake, Ozil akkungana na Aaron Ramsey, Mathieu Debuchy, Olivier Giroud pamoja na Mikel Arteta.


No comments:

Post a Comment