Sunday 22 September 2013

AFRIKA YAIPA WASIWASI FIFA!!


NI KUTOKUJUA WA SHERIA???
INATOKEA AFRIKA TU, DUNIA NZIMA HAITOKEI!!
by rahim kassonga


FIFA imepatwa na wasiwasi mkubwa kuhusu Timu za Afrika kuvunja Sheria na kuchezesha Wachezaji wasiostahili kwenye Mechi za Mchujo za Kombe la Kombe la Dunia na sasa wanataka kulishughulikia tatizo hilo ipasavyo.
Wasiwasi huo umetangazwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa FIFA Mustapha Fahmy hapo Jana.
Katika Mechi 8 za Mchujo za Kombe la Kombe la Dunia Kanda ya Afrika Matokeo ilibidi yafutwe baada ya Timu kuchezesha Mchezaji asiestahili ama kwa Sheria za Uraia au kuwa Kifungoni kufuatia kupewa Kadi katika Mechi za nyuma.
Kwenye Mechi zote hizo 8, Matokeo yalifutwa na Pointi 3 na Bao 3 kupewa Wapinzani wa Timu iliyokiuka Sheria na hilo lilileta athari kubwa kwenye Timu husika na Makundi yao.
Fahmy amesema: “Tumepatwa wasiwasi na hili ambao ni ukiukwaji wa wazi wa Sheria ambazo ziko wazi. Na hili limetokea katika Bara moja tu Duniani…Afrika. Mengine kama Ulaya, Asia na Marekani ya Kusini hamna hata tukio moja.”
Fahmy amesema kuwa inabidi wao kutafakari nini kimetokea na kutafuta ufumbuzi ili makosa haya yasijirudie tena.
Tukio la mwisho la ukiukwaji huu wa Sheria ni baada ya Cape Verde kuifunga Tunisia Bao 2-0 huko Tunis na kutwaa ushindi wa Kundi lao na hivyo kutinga Raundi ya Mwisho ya Mtoano lakini ikagundulika walimchezesha Mchezaji ambae alitakiwa kuwa kwenye Kifungo cha Mechi 4.
Cape Verde wakafutiwa ushindi na Tunisia, ambao Kocha wao Nabil Maaloul, alijiuzulu baada ya kipigo hicho, kupewa Pointi 3 na Goli 3 na hivyo wao kufuzu kuingia aundi ya Mwisho ya Mtoano ambayo itatoa Timu 5 kwenda Brazil.
Tunisia watacheza na Cameroun kwenye Raundi hiyo.
Cha ajabu ni kuwa, kwenye Kundi hilo hilo la Cape Verde na Tunisia, ni hao hao Cape Verde walionufaika walipofungwa 4-3 na Equatorial Guinea na baadae kupewa ushindi baada ya Equatorial Guinea kumchezesha Mchezaji asiestahili kwenye Mechi hiyo.

No comments:

Post a Comment