Sunday 22 September 2013

Basketball - Bryant kutocheza kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi ya NBA

by rahim kassonga


Kutokana kuwa majeruhi, mcheza kikapu nyota wa timu ya Los Angeles Lakers Kobe Bryant anaweza kusogezewa muda wa kurudi tena uwanjani mpaka atakapokuwa sawa
Hali hiyo imemfanya asionekane katika michezo ya kujiandaa na ligi hiyo maarufu kama pre season

Kobe Bryant - nyota w NBA na Los Angeles Lakers, 


Imeripotiwa kuwa Bryant amebakiwa wiki chache kabla ya kuwa fiti 100% kwa kuanza mazoezi mepesi yeye mwenyewe
Aliumia mwezi April na kuwa fiti kabisa itamchukua miezi sita hadi 8
Timu ya Lakers ilitangaza kumsajili Ryan Kelly kuziba nafasi ya Kobe kwenye kipindi hiki kigumu
Kelly amechukuliwa na Lakers mwezi june kwenye awamu ya pili ya michuano ya vyuo nchini marekani ambapo alikua kwenye Chuo kikuu cha Duke.
Wakati huo alikuwa na wastani wa pointi 12.9 na reboundi 5.3 na blocked short 1.6
Nae mlinzi wa Brooklyn Nets Deron Williams alipoongea na vyombo vya habari mjini New York amesema atakuwa sawa kuanza mazoezi nakuingia kwenye kambi mwezi October mwaka huu  japokuwa vipimo vya sumaku vinaonesha kuwa anatatizo la enka kwenye mguu wake wa kulia
Williams, ambaye alisema tatizo hilo la enka ameumia alipokuwa na Utah Jazz wiki mbili zilizopita alipokuwa akitembea na kupata tatizo linalojulikana kitaalam kama bone bruise

 


No comments:

Post a Comment