Tuesday 24 September 2013

MARIO BALOTELLI:-‘LUPANGO KWA ‘KUMTISHA REFA!!!!’

by rahim kassonga


Mario Balotelli amefungiwa Mechi 3 kwa kutumia ‘vitisho na matusi’ dhidi ya Refa mara baada ya Mechi ya Serie A Juzi ambayo Timu yake AC Milan ilichapwa Bao 2-1 na Napoli Uwanja wa kwao San Siro.
Balotelli alitolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya Mechi hiyo kwisha kufuatia kupewa Kadi ya Njano ya Pili baada ya yeye kuvaana na Mchezaji wa Napoli Valon Behrami na kisha kuanza kukwaruzana na Refa Luca Banti.
Katika Mechi hiyo, Balotelli alikosa Penati iliyookolewa na Kipa wa Napoli, Pepe Reina, na baadae kupiga shuti lililogonga mwamba na Dakika za mwisho kuifungia AC Milan hilo Bao lao moja kwa Shuti murua.
Hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kabisa kwa Balotelli kukosa Penati tangu aanze Soka la Kulipwa.
AC Milan haijasema lolote kama itakata Rufaa kupinga Kifungo hicho na kama kitabaki kama kilivyo basi Balotelli atazikosa Mechi za Serie A dhidi ya Bologna, Sampdoria na Juventus.
Wakati huon huo, Wasimamizi wa Soka huko Italy wameamuru AC Milan kufunga Jukwaa lao la Uwanja wa San Siro linaloitwa Curva Sud kwenye Mechi ijayo na Sampdoria kama Adhabu kwa Mashabiki waliokuwa wakighani Kibaguzi wakati wa Mechi waliyofungwa na Napoli.

No comments:

Post a Comment