Wednesday 25 September 2013

CAPITAL ONE CUP (KOMBE LA LIGI) LEO

by rahim kassonga


Jumatano Septemba 25
[Saa 3 Dak 45 Usiku]
Birmingham v Swansea
Manchester United v Liverpool
Newcastle v Leeds
Tranmere v Stoke
[Saa 4 Usiku]
West Brom v Arsenal
Nicklas Bendtner anatarajiwa kuichezea Arsenal kwa mara ya kwanza baada ya Miaka miwili wakati Arsenal watakaposafiri kwenda kucheza na West Brom kwenye Mechi ya Raundi ya Tatu ya Capital One Cup.
Tangu ajiunge na Arsenal Mwaka 2005, Bendtner ameshindwa kutulia na kupata Namba ya kudumu na mara 3 ametolewa nje kwa Mkopo.
Kabla Msimu huu kuanza, Bendtner alilazimika kurudi tena Arsenal baada ya kushindwa kupata Klabu ya kuhamia.
Uwezekano wa Bendtner kucheza Mechi na West Brom ulitolewa na Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambae alisema: “Jumatano tuna Mechi na West Brom A ya Capital One Cup na Bendtner ana nafasi kucheza. Kubadilisha Kikosi ni muhimu kwani Jumamosi tunacheza na kisha inakuja Mechi muhimu mno na Napoli ya UFA CHAMPIONZ LIGI.”
Mara ya mwisho Bendtner kuichezea Arsenal ni Agosti 2011 walipofungwa 2-0 na Liverpool na baada ya hapo alipelekwa kwa Mkopo huko Sunderland na Juventus.
Lakini mara baada ya kuchukuliwa kwa mkopo wa Msimu mzima na Sunderland hapo Mwaka 2011, Bendtner alitamka: “Sitarudi tena Arsenal. Ikiwa ni juu yangu, sitacheza nao tena!”


Wakati huohuo
Inaaminika kuwa Robin van Persie hatakuwepo kwenye mchezo wa leo dhidi ya liverpool baada ya kuumia kabla ya mchezo na man city jumapili

No comments:

Post a Comment