Monday 30 September 2013

UEFA CHAMPIONZ LEAGUE KESHO



by rahim kassonga

JUMANNE-ARSENAL v NAPOLI, CELTIC v BARCA, STEAU v CHELSEA! 


Mechi za Makundi-Raundi ya Pili:
Jumanne 1 Oktoba 2013
FC Basel 1893 v FC Schalke 04
FC Steaua Bucureşti v Chelsea FC
Borussia Dortmund v Olympique de Marseille
Arsenal FC v SSC Napoli
Football Club Zenit v FK Austria Wien
FC Porto Club v Atlético de Madrid
AFC Ajax v AC Milan
Celtic FC v FC Barcelona

ZIFUATAZO NI DONDOO MUHIMU ZA KILA MECHI HIZO:

KUNDI E (FC Basel v FC Schalke 04; FC Steaua Bucureşti v Chelsea FC)
• Basel na Schalke zilikutana UEFA CUP Msimu wa 2004/05 hatua za Makundi na kutoka 1-1.
• Msimu uliopita, Steaua waliifunga Chelsea kwenye UEFA EUROPA LIGI Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa Bao la Penati ya Raul Rusescu lakini kwenye Marudiano huko Stamford Bridge, Steau ilichapwa Bao 3-1 kwa Bao za Juan Mata, John Terry na Fernando Torres huku Bao pekee la Steau likifungwa na Vlad Chiricheş.
KUNDI F (Borussia Dortmund v Olympique de Marseille; Arsenal v  Napoli)
• Dortmund na Marseille zilicheza kwenye Kundi moja la UCL Miaka miwili iliyopita na Marseille kushinda 3-0 Nyumbani na 3-2 Ugenini.
• Mara ya mwisho kwa Arsenal kucheza na Timu ya Serie A ilitolewa nje ya UCL kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 kwa kuchapwa 4-0 na AC Milan huko San Siro Msimu wa 2011/12 na wao kushinda 3-0 Uwanjani kwao Emirates.
KUNDI G (FC Zenit v FK Austria Wien; FC Porto v Club Atlético de Madrid)
• Hii ni mara ya tatu kwa Zenit kucheza na Klabu za Nchini Austria na mara ya kwanza walicheza na ASKÖ Pasching ambayo baadae ilibadilishwa Jina na kuitwa SK Austria Kärnten na hiyo ilikuwa kwenye Misimu ya 2004/05 na 2005/06.
• Msimu uliopita Porto, walishinda Mechi zao zote za Nyumbani kwenye UCL kwa kufunga Bao 8 na kufungwa 2 tu.
KUNDI H (AFC Ajax v AC Milan; Celtic FC v FC Barcelona)
• Ajax walitwaa Pointi 4 kwenye Mechi za Mkundi za UCL za Msimu wa 2010/11 dhidi ya AC Milan. Wakati huo, katika Mechi ya kwanza,  Zlatan Ibrahimović aliifungia Bao AC Milan dhidi ya Ajax ambayo ilikuwa Timu yake ya zamani na Mounir El Hamdaoui kuisawazishia Ajax na kutoka 1-1 lakini katika Mechi ya Marudiano Ajax walishinda 2-0 kwa Bao za Demy de Zeeuw na Toby Alderweireld.
• Rekodi ya Barcelona dhidi ya Klabu za Scotland kwa Mechi za Nchini Scotland ni Ushindi 2 Sare 1 na Kufungwa 3.


MATOKEO-Mechi za Kwanza:
Jumatano 18 Sep 2013
FC Schalke 3 FC Steaua Bucureşti 0
Chelsea 1 FC Basel 2
Olympique de Marseille 1 Arsenal 2
SSC Napoli 2 Borussia Dortmund 1
FK Austria Wien 0 FC Porto 1
Club Atlético de Madrid 3 Football Club Zenit 1
AC Milan 2 Celtic FC 0
FC Barcelona 4 AFC Ajax 0

No comments:

Post a Comment