Tuesday 24 September 2013

Chadema wamtangazia vita Dk Mathayo David



by rahim kassonga
KILIMANJARO
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetangaza operesheni maalumu ya kumuondoa Mbunge wa Jimbo la Same Magharibi Dk David Mathayo David katika Uchanguzi Mkuu wa 2015.
Operesheni hiyo imepewa jina la Operesheni Mathayo Out kwa kifupi (OMO) imeanza wiki iliyopita kwa kufanya Mikutano ya hadhara Jimboni humo na itaendelea tena wiki ijayo.
Aidha Mmoja wa Makamanda wa Operesheni hiyo Gervas Mgonja amesema kuwa Jimbo hilo limekuwa chini ya himaya ya CCM tangu Uhuru lakini wananchi wake wapo kama wamefunga ndoa na tatizo la maji.
Dk Mathayo ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi alipoulizwa kuhusu operesheni hiyo ya kumuondoa madarakani amesema kuwa Chadema ni chama kidogo na hakimnyi usingizi kwa madai uwezo wa kampeni unaishia Himo.


EDITOR:TIDA SAIDEA

No comments:

Post a Comment