Saturday 28 September 2013

RONALDINHO KAUMIA, KULIKOSA KOMBE LA DUNIA KWA VILABU



by rahim kassonga
KOMBE LA DUNIA KWA KLABU:


NI MOROCCO 2013: DESEMBA 11 HADI 21!
STAA MKONGWE wa Klabu ya Brazil Atletico Mineiro, Ronaldinho, amechanika Musuli ya
gaucho
kwenye Nyonga na sasa yuko hatarini kuyakosa Mashindano makubwa ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu yatakayochezwa huko Morocco kuanzia Desemba 11.
Atletico Mineiro ndio Mabingwa wa Nchi za Marekani ya Kusini CONMEBOL baada ya kutwaa Copa Libertadores.
Mashindano hayo yataanza kuchezwa huko Morocco kuanzia Desemba 11 hadi 21 na kushirikisha Klabu Bingwa za kila Bara pamoja na Raja Casablanca ya Morocco ambayo imeingizwa kama Mwenyeji.


WASHIRIKI:
FIFA KOMBE LA DUNIA KWA KLABU:
Zinaanza Nusu Fainali:
-Brazil Atlético Mineiro [Brazil] Bingwa CONMEBOL
-Bayern Munich [Germany] Bingwa
Zinaanza Robo Fainali:
-Bingwa Asia HAJAJULIKANA
-Bingwa Afrika HAJAJULIKANA
-Monterrey [Mexico] Bingwa CONCACAF
Zinaanza Mchujo kabla kuingia Robo Fainali:
-Auckland City [New Zealand] Bingwa OFC
-Raja Casablanca [Morocco] Mwenyeji

Daktari wa Atletico Mineiro Rodrigo Lasmar amesema maumivu ya Ronaldinho, ambae amewahi kuzichezea Klabu za Ulaya, AC Milan na Barcelona, yanaweza kuchukua hadi Miezi mitatu kupona lakini wameshaanza kumtibu kwa bidii.

No comments:

Post a Comment