Saturday 28 September 2013

MATOKEO LIGI KUU ENGLAND



by rahim kassonga

SPURS, CHELSEA SARE, TORRES KADI NYEKUNDU!
AVB, MOURINHO WAPEANA MIKONO!
RATIBA/MATOKEO:
BPL: LIGI KUU ENGLAND
Jumamosi 28 Septemba

Tottenham Hotspur 1 Chelsea 1
Tottenham wametoka Sare Bao 1-1 na Chelsea na kuipiku Arsenal
 kileleni mwa Ligi Kuu England lakini Arsenal ambao wanacheza hii leo Ugenini wanaweza kurudi kileleni wakitoka Sare na Swansea City.
Gylfi Sigurdsson ndie alieifungia Spurs Bao katika Kipindi cha Kwanza baada ya ushirikiano mzuri kati ya Christian Eriksen na Roberto Soldado na Mpira kumfikia yeye.

MAGOLI:
Tottenham 1 - 0 Chelsea
Sigurdsson Dakika ya 19
Tottenham 1 - 1 Chelsea
Terry Dakika ya 65

Chelsea walimwingiza Juan Mata mara Kipindi cha Pili kilipoanza na frikiki yake ndio iliunganishwa na John Terry kwa kichwa na kusawazisha Bao.

Juan Mata alisaidia sana kubadilisha hali ya mchezo na kuingia kwake hakukuisaidia Chelsea kurudisha goli tu, bali pia kushambulia zaidi na kutaka kupata goli la ushindi

pengine kocha wa Chelsea leo atakuwa ameona uwezo na mchango wa Mata nakuanza kumwanzisha kwenye mechi zijazo

matokeo mengine  



 Fulham 1-0 Cardiff City


17:00 Hull City v West Ham United
17:00 Manchester United v West Bromwich Albion
17:00 Southampton v Crystal Palace
19:30 Swansea City v Arsenal
++++++++++++++++++++++++++++

++++++++++++++++++++++++++++
MSIMAMO:
NA
TIMU
MECHI
PTS
1
Tottenham
6
13
2
Arsenal
5
12
3
Chelsea
6
11
4
Man. City
5
10
5
Liverpool
5
10
6
Everton
5
9
++++++++++++++++++++++++++++
Chelsea walimaliza Mechi wakiwa Mtu 10 baada ya Fernando Torres kupewa Kadi ya Njano ya pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu zikiwa zimebaki Dakika 10 Mpira kwisha.
Sare hii imewafanya Chelsea wakamate Nafasi ya 3.
Kivutio cha Mechi hii kilikuwa mzozo kati ya Andre Villas-Boas na Jose Mourinho, Watu ambao wanatoka Nchi moja Ureno na walifanya kazi pamoja kwa Miaka 7, waliporushiana maneno lakini kabla ya Mechi kuanza walipeana mikono na mwisho wa Mechi kukumbatiana.
VIKOSI:
Spurs: Lloris, Walker, Dawson, Vertonghen, Naughton, Paulinho, Dembele, Townsend, Eriksen, Sigurdsson, Soldado
Akiba: Chiriches, Lamela, Holtby, Defoe, Chadli, Friedel, Sandro.
Chelsea: Cech, Ivanovic, Luiz, Terry, Cole, Ramires, Mikel, Lampard, Oscar, Torres, Hazard
Akiba: Essien, Mata, Schurrle, Schwarzer, Cahill, Azpilicueta, Eto'o.
Refa: Mike Dean
++++++++++++++++++++++++++++
RATIBA:
BPL: LIGI KUU ENGLAND
Jumapili 29 Septemba
15:30 Stoke City v Norwich City
18:00 Sunderland v Liverpool
Jumatatu 30 Septemba
22:00 Everton v Newcastle United  
++++++++++++++++++++++++++++

No comments:

Post a Comment