Wednesday 25 September 2013

THEO WALCOTT KUFANYIWA UPASUAJI

by rahim kassonga


FOWADI wa Arsenal Theo Walcott atakuwa nje ya Uwanja kwa Wiki kadhaa kwani Jumatano anatarajiwa kufanyiwa upasuaji wa Tumbo huko Ujerumani ili kutibu matatizo ya majeruhi aliyopata kwa ndani.
Akithibitisha habari hizi, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amekiri kuwa Walcott atakuwa nje kwa Wiki kadhaa.

Matatizo haya yatamfanya Mchezaji huyo azikose Mechi mbili muhimu za mwisho za England za kuwania kufuzu kwenda Brazil Mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambazo wanatakiwa washinde ili wajihakikishie kufuzu.
England watacheza na Montenegro Hapo Oktoba 11 na kumalizia Mechi ya mwisho ya Kundi lake na Poland hapo Oktoba 15 na Mechi zote hizo zitachezwa Wembley Jijini London.
Walcoot alishawahi kupata matatizo ya aina hii Mwezi Machi na kuwa nje ya Uwanja kwa Wiki 3.
Hata hivyo, Wenger amehakikisha kuwa tatizo la Walcott sio kubwa sana na muda mfupi baada ya Operesheni yake ataanza tena Mazoezi mepesi.

No comments:

Post a Comment