
Chama cha Demokrasia na Maendeleo -CHADEMA kinatarajia
kuanza maandamano hii leo ya kushinikiza bunge la katiba linaloendelea
mjini Dodoma lisitishwe ili kuacha kufuja fedha ambazo ni kodi ya
wananchi.
Hayo yamebainishwa jana na Mkurugenzi wa oganaizesheni na mafunzo
ya kanda wa chama hicho, Benson Kigaila wakati akizungumza na waandishi
wa habari kuhusiana na mchakato mzima wa katiba mpya.
Benson amesema takribani shilingi bilioni 47 zinatarajiwa kutumika
katika bunge hilo la katiba ambazo kama zingetumika kwenye shughuli za
maendeleo, nchi ingeweza kukua kiuchumi kwa hatua fulani.
Hata hivyo Jeshi la polisi limekwishatangaza kupiga marufuku maandamano hayo
No comments:
Post a Comment