Wednesday 17 September 2014

ODAMA LAIVU NA MUME WA MTU



Msanii nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka Odama akiwa kwenye pozi la kimahaba na anayedaiwa kuwa ni mume wa mtu.
MSANII nyota wa filamu za kibongo, Jennifer Kyaka maarufu kwa jina la kisanii kama Odama, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita alinaswa Live akiwa kwenye pozi la aina yake akiwa na pedeshee maarufu jijini Dar anayefahamika kama Papaa Daudi ambaye anadaiwa kuwa mume wa mtu.Wawili hao
walinaswa wakiwa kwenye pozi hilo ndani ya Ukumbi wa Ten Lounge uliopo Makumbusho jijini Dar es Salaam ambapo Odama alikuwa akimdekea mwanaume huyo kama mtu wake wa karibu.
Wakiwa ukumbini humo, wawili hao walionekana kupata kiburudisho kwa namna yake huku mara kwa mara wakigonga ‘chiaz’ na kunyweshana mvinyo na kuwafanya waliokuwa karibu yao kuwaonea gere.ENDELEA>>

No comments:

Post a Comment