Tuesday 23 September 2014

WHO yasema ugonjwa wa ebola unaanza kudhibitiwa Afrika.

Picha ya mfano wa virusi vya ugonjwa wa ebolaPicha ya mfano wa virusi vya ugonjwa wa ebola
Shirika la afya duniani- WHO, limesema mlipuko wa ugonjwa wa ebola nchini Nigeria na Senegal unaonekana kwisha  ingawa idadi ya vifo katika maeneo hayo kutokana na ugonjwa huo imefikia 2,800.
Ripoti kutoka ofisi ya WHO huko Afrika imesema hakuna kesi mpya za ugonjwa wa ebola zilizoripotiwa kutoka Nigeria tangu Septemba nane na hakuna hata moja nchini Senegal tangu kesi ya kwanza ya pekee katika nchi iliporipotiwa Augusti 29.
Imesema milipuko katika nchi zote umedhibitiwa. Ripoti tofauti ya WHO imesema nchi za Guinea , Liberia, na Sierra leone zinaendeelea kuripoti kesi mpya  za ugonjwa wa ebola.
Imesema idadi ya kesi huko afrika magharibi imeongezeka kufikia 5,864 na idadi ya vifo imeongezeka kufikia 2,811.

No comments:

Post a Comment