Tuesday 9 September 2014

PROMOTA ALIYEMVURUGA DIAMOND NCHINI UJERUMANI MATATANI


Promota Awin Williams Akpomiemie
Promota Awin Williams Akpomiemie

Fujo za Agosti 30, 2014 katika show ya Diamond zasababisha hasara ya euro 300,000

Stuttgart, Ujerumani – Anayejiita promota Biritts Event – inayomilikiwa na Awin Williams Akpomiemie raia wa Nigeria amejikuta katika mashaka baada ya ripoti ya polisi kuthibitsiha jumla ya hasara ya Euro 300,000 (Tsh.600 million) zilizo sababishwa na fujo ya siku ya Jumamosi 30 Agosti 2014 baada ya msanii wa Nasib Abdul aka Diamond Platnumz kuchelewa kufika ukumbini mjini Stuttgart, Ujerumani.

Baada ya uchunguzi wa polisi kufuatia fujo hizo imegundulika kuwa muandaaji wa onyesho hilo Mr. Awin Williams Akpomiemie aliudanganya utawala wa ukumbi wa Sindfingen kwa kukodisha
ukumbi huo kwa ajili ya African Party na mkutano, sio onesho la muziki kama alivyofanya na kusababisha fujo zilizotia hasara ya euro 300,000 (shilingi millioni 600=) ambazo inatakiwa alipe.
Promota huyo Awin Williams Akpomiemie hakuwa na bima ya ku-cover au kulinda onyesho hilo na ukumbi lilipofanyika ambapo ni ukumbi wa mikutano na maonesho ya bidhaa na siyo muziki.
Taarifa za uhakika zinasema kuwa polisi imelipeleka suala hilo kwa ofisi ya sheria (Stadt Anwalt) ya mji wa Stuttgart ili ichukue mkondo wa sheria. Polisi pia inaendelea  kumuhoji kwa kujihusika na biashara nyingine haramu.
Wakati huo huo, taasisi mbalimbali na jumuiya za wafrika nchini Ujerumani na jirani zimelaani vikali tabia za raia huyo wa nigeria Awin Williams Akpomiemie za kuwadanganya washabiki na kulivunjia adhi sifa za bara la Afrika nchini Ujerumani. Taasisi na jumuiya hizo zimewaonya watu kujiepusha kabisa na Mnaijeria huyo wa Britts Events, Awin Williams Akpomiemie.





No comments:

Post a Comment