Thursday 25 September 2014

REGNALD MENGI , ATWAA TUZO YA MWAKA YA MFANYABIASHARA BORA WA AFRIKA (AABLA).


http://freemedia.co.tz/daima/wp-content/uploads/2014/09/mengi.jpg
MWENYEKITI Mtendaji wa Makampuni ya IPP, Dk. Reginald Mengi, ameshinda tuzo ya Mwaka ya Mfanyabiashara Bora Afrika (AABLA), kundi la Afrika Mashariki. 

Sherehe za tuzo za AABLA, kundi la Afrika Mashariki zilifanyika Septemba 20 mjini Nairobi, Kenya na kurushwa hewani moja kwa moja na runinga barani Afrika. 
Kwa mujibu wa runinga ya masuala ya fedha na biashara Afrika (CNBC Africa), ambao ndio waandaji wa sherehe hizo, tuzo hizo za kila mwaka zimebuniwa kwa ajili ya kutambua utendaji uliotukuka katika biashara, wenye mafanikio makubwa kwenye sekta zao za biashara na vilevile kwenye jamii, ambako biashara hizo zinaendeshwa. 


Mengi ambaye alikuwa akichuana na wafanyabiashara wengine wanne wa ukanda huu wa Afrika Mashariki, mbali ya kushinda tuzo hiyo pia alipata tuzo ya mafanikio katika maisha na kusaidia huduma mbalimbali za jamii nchini. 

Dk. Mengi amekuwa mstari wa mbele katika kuchangia huduma mbalimbali za jamii kama vile kwa wasiojiweza, harakati za kupambana na kuondoa umasikini, kusaidia vikundi katika kuinua uchumi na mengine. 

Tuzo ya mfanyabiashara bora wa kike Afrika, imechukuliwa na Tabitha Karanja ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni yake ya Keroche Breweries Limited inayotoa ajira kwa zaidi ya watu 300. 

Karanja amekuwa akitoa sehemu kubwa ya faida yake kusaidia jamii na kutoa elimu kwa vijana nchini Kenya. 

Watanzania wengine waliopata tuzo hizo ni Ofisa Mtendaji wa Helvetic Solar Ltd, Patrick Ngowi, (EA Young Business Leader) na Ofisa Mtendaji wa Techno Brain Ltd, Manoj Shanker (Entrepreneur of the Year).

No comments:

Post a Comment