Thursday 25 September 2014

Obama atoa wito wa kupambana na ugaidi duniani


Rais Barack Obama akihutubia mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa New York, Marekani Sept. 24, 2014.

Rais wa Marekani Barack Obama anawasihi viongozi duniani kuungana naye katika juhudi za kulivunja nguvu na kulitokomeza kundi la wanamgambo wanaojiita Islamic State.
Katika hotuba yake Jumatano kwenye mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Marekani bwana Obama alisema kwamba kundi hilo limewauwa watu wasio na hatia nchini Iraq na Syria kwa kuwakata vichwa pamoja na kuwauwa watoto, kuzika maiti katika makaburi  ya jumla na kuyasononesha kwa njaa makundi ya kidini ya walio wachache.
Rais huyo wa Marekani alitoa mwito kwa dunia na hasa jamii ya ki-Islam kukataa kabisa itikadi ya wanamgambo wa kundi la Islamic State na al-Qaida. Alisema “saratani ya visa vya ugaidi” lazima ikomeshwe.
Bwana Obama pia alilaani “uvamizi wa Russia” katika ghasia huko Ukraine akisema Russia ni “changamoto iliyopo baada ya vita”.
Mahojiano na ingia hapa

Pia alitoa mwito wa kupanua juhudi za dunia za kupambana na mlipuko wa virusi vya Ebola ambavyo vimeuwa maelfu ya watu katika baadhi ya mataifa ya Afrika Magharibi. 
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-MoonKatibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon
Awali katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon alifungua mkutano huo kwa kusema makundi ya wenye msimamo mkali ni kitisho cha wazi kwa haki za binadamu na jumuiya ya kimataifa.
Katika hotuba yake Rais Obama alisema Marekani kamwe haitajitenga katika kutetea maslahi yake au “ahadi” za Umoja wa Mataifa zinazotetea haki za binadamu kwamba amani  inaashiria maisha bora sio tu kutokuwepo kwa vita
.

No comments:

Post a Comment